Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Jokate amsaka aliyefanya hivi kwenye Bajaj

Jokate Bajaj DC Jokate amsaka aliyefanya hivi kwenye Bajaj

Mon, 21 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MIONGONI mwa mambo yanayoweza kukufanya uishi vizuri na watu ni pamoja na upendo na kuwathamini watu wote bila kujali ni mazingira gani wanayotokea.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar, DC Jokate Mwegelo ni miongoni mwa Viongozi wanaopendwa mno na wananchi kutokana na uchapakazi wake kiasi cha wengine kufikia hatua ya kubandika picha zake kwenye vyombo vyao vya usafiri.

Sasa; kuna moja ya Bajaj zilizowekwa picha ya DC Jokate, taarifa zimemfikia mheshimiwa kiasi cha kumfurahisha mno kutokana na mtu aliyenakshi Bajaj yake kwa picha yake, jambo lililosababisha atume ujumbe kupitia kuraza zake za mitandao ya kijamii akisindikiza na picha za Bajaj hiyo;

“Nimetumiwa sana hii Bajaj, mwenye hii Bajaj namtafuta, aje ofisini kwangu tufahamiane ana zawadi yake,” amesema DC Jokate ambaye kabla ya kuhamishiwa Temeke alikuwa wilayani Kisarawe, Pwani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live