Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Gondwe aingilia kati sakata la Kizz Daniel

A3b03e09 5cba 41a7 B178 E95ac0373be3 DC Gondwe aingilia kati sakata la Kizz Daniel

Tue, 9 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe amesema Ofisi yake inafuatilia tukio lililotokea usiku wa juzi baada ya mwimbaji na mtunzi wa muziki kutoka nchini Nigeria, Kizz Daniel kutotokea kutumbuiza kwenye tamasha lililoandaliwa na Str8up vibes Masaki Dar es salaam.

DC Gondwe ameandika yafuatayo “Najua Kinondoni ndio sehemu ya Watu kupata Burudani, hatupendi jambo kama hili kutokea tena, toka limetokea Viongozi wa Kinondoni tunalifuatilia kwa karibu kazi inaendelea.

“Tunafuatilia tujue udhaifu ni wapi ili isitokee tena katika tasnia ya Burudani eneo la Kinondoni, Watu wakiahidiwa wapate thamani ya fedha yao waliolipa katika Burudani, tunalifanyia kazi kwa weledi mkubwa,” amesema Gondwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live