Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cynthia Rothrock alivyowashikisha adabu wanaume

Cynthia Rothrock Cynthia Rothrock.

Fri, 19 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mateke yake yaliyonyooka, umahiri wake wa kujikunja na kuwatandika wanaume wa shoka ilikuwa ni moja ya sifa zilizomfanya mwanamama Cynthia Rothrock akapendwa sana duniani.

Ukitaka kujua ubaya wa miguu ya mwanadada huyu, basi mkabe kwa nyuma! Ilikuwa kana kwamba miguu yake ina macho, alikuwa na uwezo wa kuzungusha mguu wake na kukupiga kwa nyuma yeye akiwa ameelekea mbele.

Umahiri wake wa mateke aliokuwa nao kutoka na kuhitimu vyema mafunzo ya sanaa za mapigano hasa staili ya taekwondo ndiyo yaliyomfanya mwigiza filamu huyu akapendwa sana duniani.

Si hivyo tu , ukakamavu wake, ushujaa na ushupavu wake uliomtofautisha na wasanii wengine wa kike katika sanaa za mapigano ni sifa nyingine za ziada zilizomfanya akapendwa sana .

Wengi wanamkumbuka katika filamu ya China O'Brien na ile ya No Retreat, No Surrender 2. Huyu ni mwenye uwezo mkubwa wa kupambana kikweli na madume yalishiba na akayashinda tena kirahisi tu!

Filamu zake alizocheza si kuigiza tu au kupewa upendeleo na waongozaji filamu, mwanamama huyu alikuwa na uwezo wa 'kiukweli' wa kufanyiza, labda tu kama nawe umepitia sanaa za mapigano unaweza kumsumbua vinginevyo watu watashindwa kujua kama umeharisha au umetapika!

Jina lake kamili ni Cynthia Ann Christine Rothrock, akiwa amezaliwa Machi 8, 1957, katika Mji wa Wilmington, Delaware, Marekani na sasa anatimiza miaka 67, akiwa na urefu wa futi 5 na inchi 3. Unamkumbuka katika filamu ipi au tukio lipi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live