Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cristiano Ronaldo kwenda Chelsea ili kupunguza gharama ya Eden Hazard

2160 Cristiano Ronaldo TZW

Mon, 29 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Klabu ya soka ya Chelsea wameripotiwa kwamba wanakaribia kumpa mkataba mpya nyota wao Eden Hazardili aendelee kukipiga Stamford Bridge lakini nyota huyo bado anawindwa na klabu mbalimbali.



Hazard ni mchezaji ambaye anahamu ya kucheza chini ya Zinedine Zidane ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Real Madrid.

Real madrid bado wanaendelea na mbio zao za kutaka kumsajili Hazard lakini pia klabu hiyo imekuwa ikiwamezea mate wachezaji wengine kutoka ligi ya Uingereza ambao ni Harry Kane na David De Gea.

Kwa mujibu wa gazeti la Don Balon , klabu ya Real Madrid wamewasiliana na chelsea kuhusu uwezekano wa kumchukua Hazard na wako tayari kumtoa Ronaldo kama sadaka katika mchakato huo. Na inasemekana kwamba chelsea wao wamekataa ofa hiyo na wamesisitiza kwamba wapo tayari kumsajili mchezaji mwenye umri wa miaka 33.



Wababe hao wa ligi kuu ya Uingereza wamependekeza kwamba kama Real Madrid watataka kubadilishana wachezaji basi wamuhusishe Marco Asensio kwenye dili hilo na sio Ronaldo.



Asensio mwenye umri wa miaka 22 kwa sasa bad hajapata namba ya uhakika chini ya kocha Zidane lakini Madrid hawpo kumuachia mchezaji huyo.

Manchester city nao ni mwiongoni mwa klabu wanaotaka kumsajii Hazard tangu walipo shindwa kumsajili Alexis Sanchez na wapo tayari kutoa kiasi cha pauni milioni 150 ili kuinasa saini ya Hazard.



Na Raheem Rajuu

Chanzo: bongo5.com