Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coy Mzungu anatoka kimapenzi na Esma? Majibu haya hapa

Esma Platnumz Coy Mzungu.png Coy Mzungu anatoka kimapenzi na Esma? Majibu haya hapa

Fri, 26 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanzilishi wa Jukwaa la Cheka Tu, Coy Mzungu ni mmoja ya watu wanaohusishwa sana kuwa kwenye mahusiano na dada yake Diamond Platnumz ambaye ni Esma Platnumz.

Akizungumzia hilo, Coy Mzungu amesema yeye ana project ya kuwanyanyua wamama wanaofanya shughuli ndogo ndogo kujiingizia kipato na kuwalea watoto wao ambao wanakuja kuwa watu wakubwa.

Amesema katika projrct yake hiyo hukutana na akina mama wa aina mbalimbali na miongoni mwa vitu ambavyo huwapatia ni vitenge ambavyo pia Esma anaviuza, kwa hiyo huenda watu wanaunga matukio na kusema anatoka kimapenzi na Esma.

Siku za nyuma Coy Mzungu alishawahi kuonekana akiwa na Esma Platnumz dukani kwake na kunyweshana juisi na mambo mengine ambayo ni viashiria kuwa wawili hao wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Mwandishi: Mahusiano yako na Esma yakoje? Coy Mzungu: No comment (akarudia tena), no comment… No comment. Mimi nina project inaitwa Special Love, lengo ni kuwatia moyo wamama wanaofanya shughuli ndogo ndogo na kipato kidogo. Naamini hawa wamama wanahitaji kutiwa moyo kwa lengo la kutambua mchango wao kwa malezi ya watoto wao ambao leo tunaona wanakuwa ma-CEO kama Diamond.

Ukiona wakina mama wanahangaika wanapata kipato kidogo, wanatumia hicho kidogo kulea watoto wao ambao baadaye wanakuja kuwa kama akina Diamond ambao wanatoa ajira kwenye kundi kubwa la vijana. Wanahitaji kutiwa moyo na kunyanyuliwa kiuchumi.

Nilianza na mama yangu mzazi, nikaenda kwa mama wengine lengo kuwafikia akina mama wengi Tanzania. Kwa hiyo ili kunogesha hilo, nikikutana nao ninawapa na vitenge ili kuafikia wamama wengi zaidi. Sijawahi kumnywesha juisi Esma, mmenifananisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live