Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coy Mzungu: Diamond hajanunua Cheka Tu, CEO anaajiriwa na kufukuzwa

Diamond Coy M.png Coy Mzungu: Diamond hajanunua Cheka Tu, CEO anaajiriwa na kufukuzwa

Fri, 26 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanzilishi wa Jukwaa la Cheka Tu, Coy Mzungu ameweka wazi kuwa licha ya staa wa Bongo Fleva na Mkurugenzi wa Wasafi media Diamond Platnumz kiandika kuwa ni CEO wa Cheka Tu, haimpi dhamana ya yeye kuwa mmiliki wa Cheka Tu.

Coy Mzungu ameongeza kuwa CEO mara nyingi huwa mwajiriwa kwenye kampuni lakini mwanzilishi ndio mmiliki hivyo watu walimtwika mzigo Diamond Platnumz

“Vyombo vya habari mnanishangaza sana, sijawahi kusoma kwenye Bio ya Diamond akiandika yeye ni CEO wa ChekaTu, mimi nikisoma naona ameorodhesha makampuni yake tu. Kwa nini Diamond mmemfanya kama mmiliki wa Cheka Tu peke yake? Ni mmoja wa wamiliki, jambo ambalo sio baya.

“Kwenye Cheka Tu mimi sio CEO, nilianzisha Cheka Tu then CEOs wakawa watu wengine. Kumbuka kuwa CEO ni mwajiriwa na muda wowote anaweza akatolewa kwenye nafasi hiyo ila mmiliki huwa hatoki kwenye hiyo nafasi. CEO ni mtu anayeweza kuajiriwa tu na kuondolewa.

“Simtoi Diamond lakini nawaelimisha watu, wakiona mtu ameweka CEO kwenye bio yake wanadhani ndiye mmiliki asilimia 100, ndio maana watu wanamtwika Diamond zigo sio la kwake. Diamond ahajanunua Cheka Tu, yuko kuhakikisha Stand Up comedy inapiga hatua, ameomba mwenyewe kama msanii kusaidia, watu wanasema amenunua.

“Diamond ni active partner wa Cheka Tu, amefanya kipande chake kwa kufanikisha muziki lakini atakalofanya lolote asimilikishwe, akifanya jambo hajanunua, ameingia Cheka Tu kuisapoti,” amesema Coy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live