Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Country Wizzy apanda thamani baada ya kujiunga na Harmonize, analipwaje kwa show..?

367C94BD 2252 4897 B523 E165782A9E90 660x400.jpeg Country Wizzy apanda thamani baada ya kujiunga na Harmonize, analipwaje kwa show..?

Fri, 5 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

Toka Rapper Country Wizzy ajiunge na record Lebo ya Harmonize ( Konde Gaing ) muziki wake umepanda thamani huku dau lake la kulipwa kwa show limezidi lile alilokuwa akilipwa kwa show za miaka ya nyuma.

Country amethibitisha hilo kwa kusema kwasasa amekuwa akipata shows nyingi tofauti na awali na kuhusu dau ni tofauti na zamani kutokana na uongozi wake wa sasa.

“Namshukuru Mungu umekuwa Mwaka Mzuri sana naona Thamani ya muziki wangu imekuwa kubwa, imenipa shows mpaka sasa nimefanyiwa Booking na ni nyingi, Show ndogo nikimaanisha local shows”

”Na international shows mpaka sasa tumepata show Tatu kwa mwaka huu, ambayo iko Tayari ni Ujerumani ambayo ilitakiwa kufanyika mwezi wa Tatu lakini kutokana na kule bado Corona ipo wako lockdown so imesogezwa, mpaka sasa nikoBooked na show 13 Za hapa ndani, Kiwango cha show siyo kibaya ni kizuri wote wanakaribishwa kuzungumza” – Country Wizzy

Ikumbukwe Harmonize alimtambulisha rasmi Country Wizzy kwenye record Lebo yake ya Konde Gaing mwezi September mwaka 2020

Chanzo: millardayo.com