Wizara ya Vijana, Sanaa na Michezo nchini Kenya imeahidi kumsaidia Rapa wa Colonel Mustafa ambaye hivi karibuni alionekana akifanya kazi ya ujenzi wa nyumba kwa ajili ya kupata pesa za kumsaidia Mama yake mzazi anayesumbuliwa na maradhi ya Kansa.
Waziri mwenye dhamana ya Vijana, Sanaa na Michezo Mhe. Ababu Namwamba alimualika rapa huyo ofisini kwake ambapo walizungumza mengi lakini kubwa ni ahadi ya kumuinua Kimuziki tena na kutengeneza pesa
“Tumesikia changamoto zako na kama Wizara, nataka nikuhakikishie kwamba tupo hapa kuongozana na wewe kwenye ukurasa huu wa changamoto. Tumekuandalia kifurushi (package) kwa ajili yako ambacho kitakusaidia kuinuka na kutembea, kufanya muziki na kutuburudisha.”
“Tunataka kukuona ukifanya Muziki tena, kuwashawishi vijana wadogo, pia kuwafundisha namna ya kuwa wasanii wakubwa. Hatua ambazo umechukua kuhakikisha Mama yako anapata huduma bora ya afya ni ya kupongezwa. Na kwa hilo, tutasimama na wewe.” Alizungumza Ababu Namwamba