Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Clouds yatoa tuzo kwa wanawake wanane

480a53283caece70e6c651add3d417a3 Clouds yatoa tuzo kwa wanawake wanane

Sun, 25 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WANAWAKE wanane nchini wamepewa tuzo mbalimbali zinazotolewa na kampuni ya Clouds Media Group (CMG) lengo likiwa ni kutoa fursa kwa wanawake kutobweteka na kuwa wabunifu, kufanya kazi kwa bidii wakiamini kuwa wanaweza.

Miongoni mwa waliopewa na tuzo hizo kwenye mabano ni Lilian Makoi (Sayansi na Teknolojia), Getrude Mligo (Malkia ajaye), Mama Jadore (Fasheni mitindo na urembo), Christine Mosha au Seven Mosha ( Burudani), Herieti Mkaanga (Tuzo ya Mwanamke Mhamasishaji) .

Wengine waliopewa Tuzo ni Neys Cassava ( Biashara ya Chakula), Rose Swai ( Kilimo- Biashara) Profesa Paulina Mella, ( Afya na Ustawi wa Jamii) na Innocesia Masawe alipata Tuzo ya Heshima katika sekta ya Michezo.

Akizungumzia tuzo hizo , Mkurugenzi wa Biashara, Sheba Kusaga aliwataka wanawake kuthubutu badala ya kusubiri kuwezeshwa.

“Natamani ule ujumbe alioutoa Rais Samia juzi kule bungeni kila mwanamke autambue, ni pale aliposema Mungu hakuumba akili ya mwanamke dhaifu bali wote wanawake na wanaume wako sawa,” alisema Sheba na kuwataka wanawake kupambana kwa bidii.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo, Mligo ambaye ni kijana, aliahidi kuwa hatowaangusha watanzania kwa kuwa ni mbunifu katika kutengeneza programu tumizi zikiwemo zile zenye kuhimiza kusoma.

Profesa Mella alishukuru kutambuliwa licha ya kuwa ni miaka mingi tangu alipoanzisha Shahada ya Uuguzi tangu mwaka, 1989 na alishastaafu.

“Ninawashukuru wanafunzi wangu , wameleta sifa katika nchi ya Tanzania, wamesoma na wanajielewa wanajua wanachofanya, wameenea hapa nchini,” alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz