Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Clouds Media hawajanisaidia kitu - Chid Benz

Chid Benz Hds Clouds Media hawajanisaidia kitu - Chid Benz

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Hip Hop Chid Benz ameendelea kuelezea jinsi watu na baadhi ya taasisi zinavoigiza kuwa zina huruma na maisha yake anoishi kumbe ni unafiki wanafurahia anguko lake

Chid amesema watu wengi hawana huruma na maisha yake wanaigiza tu huko mitandaoni kuwa wanania ya kumsadia huku akienda mbali zaidi na kukitolea mfano kituo cha Clouds Media kilichofanya naye mahojiano hivi karibuni na kuibua mijadala mingi kuhusu maisha anayoishi msanii huyo ambapo amedai kuwa kituo hicho hakikumpa msaada wowote baada ya mahojiano yale.

“Ngoja nikwambie mdogo, Mwasiti nilimkuta Studio za 41 Record kwa Lamar wakati naenda kurekodi wimbo wangu na K-Lynn. Mwasiti akasema ilikuwa arekodi wimbo wake na Profesa jay kama mbadala wangu baada ya kuambiwa na Bosi Ruge kwamba kumpata Chid ni ngumu, mimi nilirekodi naye lakini mbona hanipigii simu?

"Alikiba nimefanya naye ngoma kama mbili au tatu, akaachia albamu yake, mbona hanipigii kwamba broo hivi na hivi nakusaidia hivi? Hawa watu hawana huruma na mimi

"Mfano Clouds Media yenyewe si ndiyo ilifanya yale mahojiano na mimi, kwa nini Boss wa kile kituo baada ya yale mahojiano yao hakunifata na kuniuliza nini nataka anisaidie, aniulize kwanza naishi wapi?

"Inamaana mimi sijawahi kufanya mema kwa Clouds Media? Sikatai Clouds wamenisaidia, nazungumzia suala la hali hii niliyo nayo sasa. Shoo ngapi nimefanya mimi pale ndiyo maana naumia ukiniambia watu wanayaonea huruma maisha ninayo ishi,“ alisema Chid Benz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live