Bodi ya filamu nchini Tanzania imewafungulia kesi polisi waigizaji wa vichekesho, Stering Makoti @kicheche_ na Ridhiwani Juma @clamcris_ kwa makosa ya kurusha maudhui yanayoenda kinyume na maadili.
Inadaiwa waigizaji hao walitakiwa kuwa wanapeleka kazi zao bodi ya filamu zihakikiwe kabla ya kutoka lakini wamekuwa wakikaidi kanuni hizo.
Inadaiwa siku ya jana waigizaji hawa walikamatwa na polisi, endelea kufuatilia Manara TV kwa taarifa zaidi kuhusu sakata hili.
“Wamekiuka sheria ya filamu (michezo ya kuigiza), sheria yetu iko wazi, ukifanya kosa kwa mara ya kwanza unapigwa faini ya papo kwa papo ambayo haizidi Tsh milioni 1, ukikaidi unapigwa faini ya Tsh milioni 10 mpaka Tsh milioni 12, ukikaidi tunakupeleka mahakamani. Ka hiyo tupo katika ngazi hizo tatu, mpaka unakamatwa maana yake umekiuka ngazi zote tatu.
“Hao wasanii wanendelea kupandisha video zao YouTube bila kufuata taratibu, sheria na kanuni za Bodi ya Filamu. Mwanzoni tulichukua jukumu la kuwaita, kukaa nao na kuwapa elimu kuhusu sheria hizi, tuliwaambia wanatakiwa walete hizo clip zao walizopandisha YouTube ili zihakikiswe na kupewa vibali.
“Pia, wao kujisajili kama wadau wanaofanya masuala ya filamu. Mara ya kwanza walikubali wakaandika maelezo na kukubali kuleta video zao ili zihakikiwe waendelee na shughuli zao.
“Ikapita miezi miwili, mitatu, mine mpaka sita, tukajaribu kuwaita tuzungumze nao wakawa hawapokei simu na hawataki kutoa ushirikiano. Bodi ikaenda kutoa ripoti polisi kwamba kuna hawa watu wamekaidi na hawataki kutoa ushirikiano, ndipo wakakamtwa," imesema Bodi ya Filamu.