Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cilian Murphy kurejea tena kwenye Peaky Blinders

Murphy Kuonekana Kwenye Peaky Blinders Cilian Murphy.

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji Cilian Murphy, ambaye hivi majuzi alishinda Tuzo ya Academy (Academy Awards) kama Muigizaji Bora kwa uhusika wake katika filamu ya "Oppenheimer," atachukua nafasi yake kama Tommy Shelby katika muendelezo ujao wa Filamu ya "Peaky Blinders"

Filamu hiyo, iliyopangwa kuanza kurekodiwa mnamo Septemba 2024, itaendelea na hadithi ya Familia ya Shelby na genge la Peaky Blinders katika uongozi wa Vita vya Kwanza vya Kidunia.

Muandaaji wa filamu hiyo Steven Knight amethibitisha kuhusika kwa Murphy na kusifu talanta kubwa na taaluma ya mwigizaji huyo, akisema kwamba Murphy anastahili yote kutambuliwa kwa kazi yake iliyo bora.

Murphy mwenye umri wa miaka 48,amejizolea umaarufu kote ulimwenguni kwa uhusika wake katika filamu mbalimbali hususani hii ya"Oppenheimer"na "Peaky Blinder"

Je, Ulimkubali kwenye Filamu gani huyu mwamba?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live