Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Chukua hatua hizi kama unampenda mtu hakupendi

Chukua Hatua Hizi Kama Unampenda Mtu Hakupendi Chukua hatua hizi kama unampenda mtu hakupendi

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Asikwambie mtu, maumivu ya kumpenda mtu halafu yeye akawa hakuelewi huwa yanauma sana. Unateseka kisaikolojia, unafanya kila unalotakiwa kufanya ili aweze kuelewa lakini mwenzako wapi. Ni kama vile unampigia mbuzi gitaa, hachezi yeye anabaki anakutazama tu.

Najua hii inawakuta sana wanaume ambao kiasili ya Mtanzania mara nyingi wao ndio huanza kueleza hisia zao lakini hata wanawake pia huwa inawatokea. Mwanaume anatuma meseji ndefu halafu majibu yanakuja yale mafupimafupi; ok, yeah, pow na mengine mengi yanayofanana na hayo.

Mwanaume anajaribu kujizungumzisha maneno mengi, akitegemea kupata majibu yenye kutia moyo lakini badala yake anaambulia majibu mafupi na yenye kukatisha tamaa hata ya kumzungumzisha kwa mara nyingine. Hapo ndipo mapenzi yanapogeuka mateso. Ndugu zangu, inapotokea hivyo jua kuna sababu. Yawezekana akawa unayemhangaikia ana mtu wake. Anamheshimiwa aliyenaye, haoni sababu ya kumuacha yeye na kuwa na wewe.

Hoja yangu hapa ni nini? Unapaswa kujua kwamba mahusiano mazuri huwa yanajileta yenyewe. Huwezi kutumia nguvu nyingi sana kulazimisha. Huwa yanatokea kama ajali. Utashangaa tu siku ambayo hujatumia hata nguvu nyingi lakini inatokea tu.

Siku hiyo hata wewe mwenyewe utashangaa jinsi utakavyoona mambo yanajipa kirahisi wakati kuna mahali ulitumia nguvu nyingi bila mafanikio. Kuna mahali ulipenda, ulitumia nguvu nyingi lakini uliambulia patupu.

Tumia kila aina ya ushawishi unaojua kumfanya mtu unayempenda awe wako. Yawezekana akakuonesha majibu ya mkato ya kukatisha tamaa, yawezekana akakujibu majibu ya dharau, lakini wewe usikate tamaa.

Heshimu hisia zake na dunia hii haijaisha wachumba, ipo siku utakutana na mwingine ambaye hata hatakuzungusha, hatakusumbua na ukisema mara moja tu anakuwa ameshakuelewa sababu huyo ndiye ambaye mnaendana.

Huyo ndiye ambaye ‘damu’ zenu zinafanana. Huyo ndiyo mwenzi wako wa maisha na mkianzisha maisha ya uhusiano, mtadumu miaka mingi!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live