Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chuchu achana na mume wangu - mke wa Lukamba

Zc Chuchu Luka Chuchu achana na mume wangu - mke wa Lukamba

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanadada anayefahamika kama 'Pendeza' ameibuka kwenye vyombo vya habari na kumpa onyo kali Mwigizaji Chuchu Hansy aache kumtongoza mume wake Lukamba haraka iwezekanavyo.

Pendeza ambaye awali alikuwa akionekana kwenye Tamthilia ya Jeraha ya Chuchu Hansy na Ray Kigosi, amesema kwa sasa haonekani tena kwenye Tamthilia hiyo baada ya kugundua Chuchu alikuwa anamnyemelea mpenzi wake Lukamba kwa kumtumia meseji za kuchombeza akitaka tuvitu-vitu twa siri kutoka kwa Lukamba.

Siyo yeye tu, hata Lukamba ameacha kuonekana kwenye Tamthilia hiyo na chanzo kikubwa kikiwa ni hichohicho.

Amesema alikuta meseji za Chuchu kwenye simu ya Lukamba akimwambia atampatia kila kitu kama atamkubali, amesema alikuwa anampa ahadi kwamba yeye ni Mtanga anayajua mapenzi vizuri, atampa kila kitu atakachotaka ikiwa ni pamoja na kumnyunyuzia zawadi za hapa na pale.

Pendeza ameendelea kusema Chuchu alikuwa anamuonea wivu kutokana na uzuri alionao akahofia Ray angeweza kumtamani na kutembea nae, ameongeza kuwa Chuchu Hansy ameshazeeka sasa, na kama alishindwa kula raha ujanani aache kumsumbua Lukamba kwasababu hana muda na wazee, aendelee na mzee mwenzake Ray Kigosi ambaye pia hajatulia kwani hata yeye alikuwa anamdokezea ili aonje penzi lake kisiri-siri.

Ameongeza kuwa, Chuchu ni mbahili na pesa zake kwani awali alitaka kumlipa elfu tano kama wanavyolipwa waigizaji wengine wa Tamthilia hiyo lakini alikataa na kuwapa onyo kwamba yeye anajiweza kifedha, anamiliki gari hawezi kupewa elfu tano, ndipo Chuchu akawa anamlipa elfu 50 ya mafuta, haikumtosheleza ila alimuonea huruma akaamua kuichukua lakini pia alikuwa hali chakula kambini kutokana na upishi mbovu wa chakula hicho cha Chuchu.

Hata hivyo kwenye mahojiano na Azam TV, Chuchu alipoulizwa sababu za kuwaondoa wasanii hao kwenye Tamthilia yake ya Jeraha, Chuchu alisema aliamua kuwaondoa kutokana na utovu wa nidhamu ikiwemo kuchelewa kazini ambapo walikuwa wanafika kazini muda wanaojisikia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live