Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chuchu Hans aeleza alivyopata ugumu kumpata Ray aigize naye

CHUCHU NA RAY Chuchu Hans aeleza alivyopata ugumu kumpata Ray aigize naye

Wed, 29 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chuchu Hans ni staa na mtayarishaji wa filamu nchini Tanzania ambaye kwa sasa anatamba na tamthilia yake mpya ya Jeraha.

Chuchu Hans amefunguka jinsi alivyopata wakati mgumu kumpata baba mtoto wake ambaye naye ni muigizaji na mtayarishaji mwenzake wa filamu, Ray Kigosi ili aweze kushiriki kwenye tamthiliya yake hiyo.

Mwanamama huyo amesema kuwa, kwa sasa yeye na Ray wanalea mtoto wao na zinapotokea kazi basi hushirikiana kwa pamoja kwa kuwa wote wanafanya kazi za aina moja.

Chuchu ameyasema hayo wakati akifuturisha watoto pamoja na wadau mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live