Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chuchu Hans: Sikumtaja Ray makusudi shukurani za ujauzito

36345 Pic+chuchu Chuchu Hans: Sikumtaja Ray makusudi shukurani za ujauzito

Sat, 12 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Msanii wa filamu nchini, Chuchu Hans amefafanua kwa nini hakumtaja mzazi mwenzake, Vicent Kigosi maarufu kama Ray miongoni mwa watu waliomsaidia wakati wa ujauzito kwa sababu hakuwa karibu naye.

Chuchu ametoa maelezo hayo baada ya kuwataja watu waliomsaidia na kuwa karibu naye kipindi cha ujauzito wa mwanaye Jaden wakati akimtakia heri ya siku ya kuzaliwa na kuacha kumtaja baba yake, Ray.

Katika maelezo yake, Chuchu alisema ni kweli Ray hakuwa na mchango wowote kwa sababu mimba yake haikuwa ikipatana na mzazi mwenzake huyo kiasi cha kuwa mbalimbali katika kipindi cha kuelekea kujifungua.

“Watu wanaweza kudhani nilisahau kumtaja katika watu ambao walikuwa msaada kwangu katika kipindi hicho kigumu nilichopitia, lakini la hasha. Nilifanya kusudi na hata yeye anajua kwa nini sijamtaja ni kwa kuwa alikuwa mbali na mimi na kwa nini nimpe sifa za uongo,” alisema.

“Wanaojua kuhusu mimba wanalifahamu hili, kuna wakati inaweza kukuweka mbali na watu wanaopaswa kukusaidia kwa sababu huwapendi.”



Chanzo: mwananchi.co.tz