Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chrisean achora tattoo ya Blueface

Chrisean Achora Tattoo Ya Blueface Chrisean achora tattoo ya Blueface

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chrisean ame-share video ikimuomesha akiwa na tattoo ya Blueface usoni. Ikumbukwe Chrisean aliwahi kuchora tattoo ya blueface shingoni na kuifuta kutokana na migogoro iliyokuwa ikiendelea kwenye mahusiano yao na kupelekea kuachana , sasa amerudia tena kuchora Tattoo nyingine.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram @chrisean ameweka video hiyo inayomuonyesha akichora Tattoo ya rapa huyo na kuweka caption ya kupaza sauti ili Blueface aachiwe na kusindikiza na neno Nakupenda.

Blueface anatumikia kifungo cha zaidi ya miezi 6 jela ya Los Angeles kwa kosa la kukiuka masharti ya dhamana katika mashtaka yake ya kuhusika kwenye tukio la upigaji wa risasi huko Las Vegas 2022 lakini pia kumshambulia baunsa katika club ya los angeles 2021 hivyo ameripotiwa kuwa atakaa jela hadi msimu wa majira ya joto (Julai 2, 2024).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live