Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chris Brown na Lil Baby kuiteka Marekani nzima

Chris Brown And Lil Baby One Of Them Ones Tour Chris Brown na Lil Baby

Wed, 27 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii marufu duniani, Chris Brown na Lil Baby wanatarajia kufanya ziara ya pamoja ya mfululizo wa maonyesho kadhaa katika msimu huu wa joto huko nchini Marekani, wakianza na shoo kubwa huko Raleigh.

Ziara hiyo iliyopewa jina la ‘The One of Them Ones’, inatarajiwa kuanza mapema Julai 15, na kuendelea hadi Agosti 27, 2022 ambapo watazunguka katika maeneno mbali mbali ikiwamo New York City, Toronto, Chicago, Atlanta, Los Angeles, Las Vegas.

Taarifa za ziara hiyo zimekuja siku chache baada ya kutolewa kwa video rasmi ya Ed Sheeran ‘2step’ remix akimshirikisha Lil Baby , ambaye pia mwezi huu alishiriki jozi ya video mpya za solo ikiwa ni pamoja na kutumbuiza kwenye tamasha la Coachella kama sehemu ya kujirejesha vyema kwenye sanaa.

Nje ya ujio wa ziara hiyo, kwa upande wa Chris Brown, wiki hii yeye alitangazwa kushirikiana na Renowned’s John Dean kwenye mradi wa NFT unaoitwa The Auracles.

Pia mwezi huu, Brown alishiriki wimbo wake mpya uitwao “WE (Warm Embrace),” uliotayarishwa na Don City. Wimbo uliotanguliwa na ‘Iffy’ alioutoa mapema Januari 2022.

Chris brown na Lil baby si washindani kimuziki, lakini kuna funzo kubwa kwenye ushirikiano baina yao, hasa kwenye kutengeneza pesa kupitia talanta zao, kibongo bongo ni mara chache kusikia aina ya ziara za namna hii zenye kuwahusisha wasanii wanaofanya vizuri kwa pamoja.

Jambo ambalo pengine likitazamwa linaweza kuleta mwamko mkubwa kutokana na nguvu kutoka pande mbili za wasanii kukutana pamoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live