Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chris Brown afunguliwa Mashtaka

Chris Brown Album 11.jpeg Chris Brown

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la #AbeDiaw amemshitaki mwanamuziki Chris Brown kwa madai ya kumpiga na chupa kichwani mwezi #Februari, katika club ya Tape nchini Uingereza.

Kwa mujibu wa TMZ inaeleza kuwa kufuatia na ‘kesi’ hiyo #Diaw anadai #Chris alitumia chupa kama silaha na kumpiga kichwani na kusababisha kupoteza fahamu (kuzimia).

Aidha mshitaki huyo amedai kuwa polisi jijini #London wana video na ‘picha’ zikimuonesha #Chris akimpiga mtu huyo hivyo basi anamshitaki msanii huyo kwa ajili ya fidia.

Kwa upande wa mwanamuziki huyo hajazungumza chochote kuhusiana na tukio hilo mpaka sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live