Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chris Brown achafukwa, awalipua AMAs Awards

Chris Brown Michael Jackson AMAs Chris Brown na Michael Jackson

Wed, 23 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki nguli tokea nchini Marekani @chrisbrownofficial ameendelea kuiweka kikaangoni Kamati ya maandalizi ya tuzo za America Music Awards baada ya kufuta show ya msanii huyo iliyotakiwa kufanyika kwenye kilele cha tuzo hizo, Jumapili ya Novemba 20.

Shoo ya Breezy ilikuwa ni mahususi kwa ajili ya Legacy ya Michael Jackosn kupitia wimbo wake wa Thriller uliokuwa ukitimiza miaka 40 tangu utoke.

Bahati mbaya na kitendo ambacho kiliendelea kukoleza wino kwenye uvumi kuwa Breezy anabaniwa kwenye majukwaa ya tuzo na lengo ni kuona anapotea kabisa.

Ni baada ya Kamati ya Tuzo hiyo kuifuta shoo ya Chris siku moja kabla, huku msanii huyo akiwa amefanya maandalizi yote.

Inadaiwa kuwa hafla ya Tuzo ilitazamwa na zaidi ya watu milioni 3 duniani kote, ili kuonyesja ukubwa wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Chris Brow ameamua kupakia video nzima ya maandalizi ya show yake kwenye tuzo hizo ambayo imefikisha zaidi ya watazamaji milioni 12, mara 4 ya watazamaji wa AMAs.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live