Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chris Brown aamrishwa kulipa mkopo wa Bilioni 4

Chris Brown Album 11.jpeg Chris Brown

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki Chris Brown huenda akapoteza vitu vyake vya thamani ikiwemo jumba lake la kifahari na mali zake nyingine , Hii ni baada ya Mahakama ya mjini Los Angels kuamuru staa huyo kulipa deni la $1.7M sawa na Tsh.Bilioni 4.3+ alizokopa katika benki ya City National kwa ajili ya kununua migahawa miwili ya 'PopeyesChicken '

Breezy licha kuchukua mkopo huo kwa ajili ya kununua migahawa hiyo hakufanya hivyo na alishindwa kulipa deni hilo, ChrisBrown inamlazimu kulipa deni hilo kutokana na kesi iliyofunguliwa na Benki hiyo Mjini Georgia ambapo alishtumiwa kwa kushindwa kutimiza ahadi yake inayohusiana na uwekezaji.

Staa huyo ana siku 30 pekee za kujibu na kukamilisha taratibu zote za deni hilo na endapo atashindwa basi atakuwa hatarini kupoteza vitu vyake vya thamani kama Nyumba na mali zake nyingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live