Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chino: Msinifananishe na Diamond, mnaniharibia!

Chino Kidd (2).jpeg Chino: Msinifananishe na Diamond, mnaniharibia!

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moja ya Wasanii wanao trend kwa sasa Bongo ni Chino Kidd, ambaye ameachia amapiano kali sana ambazo zimekuwa zikihiti kiasi ambacho ukienda Klabu ukisikia "Chino Wana Man" huwezi kukaa kwenye meza.

Chino amezungumza na waandishi wa Habari kitendo cha yeye kufananishwa na Diamond lakini pia kufananishwa na Marehemu Costa Titch kutokana na staili yake ya uchezaji lakini pia kuimba kwake Amapiano.

Chino ambaye ni mnenguaji na sasa ameingia kwenye muziki amesema ni kweli yeye ni msanii mzuri na anafanya vizuri kwa sasa, lakini hapendezwi na kitendo cha mashabiki kumshindanisha na wasanii wakubwa waliomtangulia wakiwemo Diamond Platnumz Costa Titch na wengine wengi.

Amesema hii inamuharibia kwasababu bado anahitaji msaada na sapoti kubwa kutoka kwa kaka zake hivyo wanapomshindanisha wanamuharibia kwasababu wanamtengenezea chuki baina yake na wasanii wakubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live