Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chino Kidd amshukuru Marioo

Chino Marioo Chino Kidd amshukuru Marioo

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Chino Kidd kuachia kionjo cha Wimbo wake "Change Vibe" aliomshirikisha Rapper Stamina pia ametumia fursa hiyo kushukuru watu wote ambao wamekuwa wakimuunga mkono katika safari yake ya muziki.

"Cha kwanza nianze na kuwashukuru kwa dhati watu wote kwa upendo mkubwa mlionionyesha juu yangu na kufanikisha kuokoa maisha yangu na familia yangu nianze na boss wangu Marioo management nzima ya Bad Nationtz na Wanaman gang ikiongozwa na mwanangu @cweder_tza na viongozi wengine wote waliojitolea na kujaribu kunisaidia kwa namna moja au nyingine.

Niwe mkweli tu safari yangu hii mpya imesaidiwa na watu wengi sana na wa kila aina: Dancers, watoto, watu wazima, wamama, media zote, waandishi wa habari, Presenters, ma Dj, ma producers wakiongozwa na kaka yangu S2Kizzy

Nimesema haya yote kwa sababu sihitaji nije kulaumu au kujutia kwenye maisha kwa hili jambo kubwa ambalo lipo wazi na ni la kweli limefanyika kwenye maisha yangu.

Nawashukuru sana sina cha kuwalipa ila Mungu pekee atajuwa jinsi ya kuwalipa japokuwa changamoto huwa hasikosekani ila naamini na mimi katika mafanikio yangu nitajitahidi kurudisha kwa jamii hata kwa asilimia kadhaa Asanteni na nawaomba mnipokee tena kwenye ukurasa huu mpya wa muziki asanteni sana," amesema Chino Kidd kupitia Ukurasa wake wa Instagram.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live