Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chino Kid amvaa Shetta 'ametukosea sana'

Chino Kid Na Shetta Chino Kid amvaa Shetta 'ametukosea sana'

Thu, 17 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii anayetamba kwenye anga la Amapiano, Chino Kid, amejilipua na kumwambia bro wake kwenye gemu, Shetta kuwa amekosea sana kuudiss muziki wa Amapiano.

Chino amesema, kitendo cha yeye kurudi kwenye gemu na kudiss muziki ambao unawapa watu riziki sio jambo la busara kwa msanii mkubwa kama yeye.

"Yeye kama alikuwa anakuja kwenye gemu hakuwa na sababu ya kudiss Amapiano, angefanya muziki wake na watu wangempokea. Unapodiss muziki ambao kuna Ma-DJ wamepata umaarufu kwa kupiga huo muziki, kuna wasanii wanafanya vizuri ni kuwakosea," alisema Chino.

Jana na juzi, Shetta aliandika kupitia Insta Story yake kuwa muziki wa Amapiano haufiki mbali na haupigwi kwenye klabu za Sauz ambako ndiko kwenye chimbuko la muziki huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live