Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chino Kid ahamishiwa Hospitali ya Muhimbili

Chinoooo WA0015 Chino Kid ahamishiwa Hospitali ya Muhimbili

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Nabeel ambaye alikuwa dereva kwenye gari lililombeba mwanamuziki na mnenguaji, Isaya Mtambo maarufu ‘Chino Kid’ pamoja na wenzake, amefariki dunia kufuatia ajali ya gari iliyotokea siku ya jana.

Asubuhi ya jana Mtayarishaji wa muziki ‘Abbah Process’ amethibitisha taarifa hiyo ya masikitiko ambapo amesema wamempoteza mwanafamilia mwenzao ambaye amemtaja kwa jina la Nabeel.

Hata hivyo inadaiwa kuwa Chino amepata majeraha sehemu ya kifua na sasa yupo Hospitali ya Taifa Muhimbili huku baadhi ya ‘madansa’ wake wakidaiwa kuvunjika miguu.

Ajali hiyo ilitokea juzi Jumamosi Novemba 11, 2023 eneo la Kabuku mkoani Tanga ambapo gari lao aina ya Toyota Alphard liligongana na lori la mafuta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live