Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chidi Benz afunguka siri nzito ya Pancho Latino

Srg Chid Pancho Chidi Benz afunguka siri nzito ya Pancho Latino

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

King Kong, Rashid Makwiro maarufu kama Chidi Benz humwambii kitu kuhusu marehemu Pancho Latino sababu alikuwa mmoja wa ma-producer ambaye alienjoy sana kufanya naye kazi pia alimbless ngoma ya Dar es Salaam Stand UP.

Chid amefunguka hayo wakati akizungumzia kuhusu producers anaowakubali Bongo na ana-enjoy kufanya nao kazi kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa ngoma zake.

“Marehemu Pancho ndiyo producer niliyemuelewa zaidi, ingawa maproducer wote na-enjoy lakini hata wao ukiwauliza watakuambia wanafurahia kufanya kazi na mimi. Lazima nimtaje Pancho kisha Allen Mapigo kwa sababu nilifanya nao ‘Dar es Salaam Stand Up’.

“Lazima ikumbushe watu kwamba dar Stand Up alifanya Pancho, akaja kufanya mixing Allen Mapigo, japo tulianzia kwa Dully, lakini maproducer wote nafanya nao vizuri.

“Kwa sasa ninafanya na S2Kizzy, ninafurahia pia na ninaona watu wengi wanafanya kwake, hivyo naona waooh, hii game ya sasa nikiingia humo ndani nakutana na vijana mabo kwa sasa ndiyo wameshika laini,” amesema Chidi Benz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live