Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chid Benz ampigia salute Fid Q "Umeonesha ukomavu"

Fid Q Chid.jpeg Chid Benz ampigia salute Fid Q "Umeonesha ukomavu"

Sun, 27 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa Chid Benz ameonesha kufurahishwa na mwenendo wa rapa mwenzie Fareed Qubanda maarufu Fid Q  kufuatia namna alivyoweza kushughulikia na kutafuta suluhu ya sakata la uteuzi wa Steve Nyerere kama msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania.

"Farid I like the fact umeweza control na kuonesha yaliyo ndani yako busara, heshima, bila kuwa mbinafsi wala kukebehi mtu au watu huu ndiyo ukomavu uliyo ndani yako.

Haijalishi mapungufu yaliyojitokeza (KAMA YAPO) umesimama kweli G. Hatukatai kwenye game kuna sintofahamu nyingi za kukatisha tamaa especially now na yanazidi kujitokeza siyo point yangu ya sasa."

Chid Benz ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuchapisha ujumbe huo kama sehemu ya kuuthibitishia umma alichokiona kwa Fid Q katika kipindi chote cha changamoto hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live