Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chid Benz amechafukwa, azidi kumuwashia moto Diamond

Chidi Benz Ft Diamond Platnumz Chid Benz azidi kumuwashia moto Diamond

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa hip hop Bongo, Rashid Makwiro 'Chid Benz'amefungukua na kudai kuwa hakupata kitu baada ya Diamond Platnumz kuingiza mstari kwenye wimbo wake mpya uitwao ‘Tunaishi Nao’, uliotoka miezi miwili iliyopita.

Chidi ameeleza kuwa pamoja na kuahidiwa vitu vingi ikiwemo kufanya promo na msanii huyo baada ya kufanya wimbo huo lakini hadi wimbo umetoka hajapata hata mia na hajafanya video ya wimbo huo mpaka sasa.

"Mimi nilikwenda kurekodi kwa S2Kizzy. Diamond aliufuata wimbo wangu studio na kurekodi bila ridhaa yangu. Mimi niko zangu maskani nimetulia nakula zangu kitu sin ahata mia masikini kumbe Diamond anatrekodi wimbo wangu studio, ningejua ningeenda studio niwakute wamejaa wanipe hata laki.

"Baadaye nikaambiwa hii ni kama sapraizi, Diamond amerekodi korasi ya wimbo wako, nikasema hapana. Ninampenda Diamond, ni mdogo wangu naweza kuita ni mtoto wangu na yeye anajua hata akikaa na familia yake.

"Sawa ni sapraizi na Diamond, huyu ni msanii namba moja Tanzania ninavyoona mimi, kimaendeleo. Akatangaza Mwanza kwamba Chid atakuwa hiv, hii ngoma itakuwa promoted, bro apewe promotion mimi nitampa hiki na hiki, mimi nikafurahi na mapombe yangu.

"Halafu baadaye hamna kitu chochote kuhusu hayo yaliyosemwa, sitaki kufuatilia, nilikutuma ukarekodi wimbo wangu studio? Kama nilitaka kumshirikisha Banana Zoro, au Linah, au Ali Choki, vipi wewe uende kurekodi huo wimbo ambao mimi sikufanya korasi.

"Sijalipwa hata shilingi mia, wimbo wangu, idea yangu, maandishi yangu, nilitembea kwa mguu kutoka Ilala mpaka Sinza kwa S2Kizzy kila kitu mimi, inarekodiwa, inawekwa korasi na msanii miubwa na sipati hata mia na sishutiwi video, jamani mimi nimefanyaje, nimeharibu labda?" amesema Chid Benz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: