Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chid Benz afunguka kuhusu Manara

Manara Chid Benz Chid Benz afunguka kuhusu Manara

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki Chid Benz amefunguka kuhusu suala la CEO wa Manara TV, Haji Manara kutaka kumsaidia kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya.

Akizungumza na Manara TV, Chid Benz amesema anamshukuru sana Manara kwa moyo aliyoonesha kutaka kumsaidia kwani kuna wasanii wengi aliyowahi kuwasaidia huko nyuma lakini hawajamuonesha upendo hata wa kumpigia simu wala kumtumia messege kama alivyoonesha Haji Manara.

“Haji Manara alichokosea ni kitu kimoja tu kusema kwamba hana uwezo wa kunipata mimi wakati mimi napatikana muda wote ila kwa upande mwingine namuelewa anaweza kumuomba msanii namba yangu na huyo msanii akamnyima makusudi sababu hanipendi mimi,“ alisema Chid Benz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live