Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chid Benz: Ruge ameondoka na ‘Password’

44133 Pic+chidii Chid Benz: Ruge ameondoka na ‘Password’

Wed, 27 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro maarufu kwa jina la  'Chid Benz’ amesema marehemu Ruge Mutahaba ameondoka na Password.

Chid Benzi ameyasema hayo leo Jumatano, Februari 27,2019 alipokuwa akizungumzia mchango wa Ruge katika muziki kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi.

Msanii huyo aliyewahi kutesa na wimbo wa Dar es Salaam Stand up, amesema Mkurugenzi huyo wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, ameondoka na password ya muziki na mpaka kuifungua itachukua takribani miaka saba.

“Kuna vitu Ruge alivitawala kwenye muziki na mpaka atokee mtu avijue sio leo wala kesho kwa kuwa vingi alikuwa akivifanya mwenyewe, kiukweli tumepoteza mtu wa muhimu,” amesema msanii huyo.

Kuhusu watu wanaomsema vibaya, Chid  amewaita wapumbavu kwa kile alichodai hakuna msanii ambaye hajawahi kudhulumiwa kwenye maisha ya muziki na kutaka wanayemuongolea vibaya waulizwe vizuri wamedhulumiwa nini au wanawake?

“Watu kama sisi tushadhulumiwa, tushatapeliwa , tumepata mahela, tumevuta madawa tumeacha yaani tumefanya vitu vingi kwenye muziki lakini bado tunamuona Ruge mzuri, huyo anayesema katapeliwa amemchukulia mwanamke au muulizeni vizuri”.

Ameendelea kueleza kuwa Ruge amefanya vitu vingi katika muziki na anaamini watu walikuwa hawajui namna anavyofanya hadi leo kuacha alama na watu kumlilia.

Hata hivyo, Chid Benz amesema kwenye muziki kunahitaji watu tofauti na kuhoji kwamba hivi leo angekuwepo Shigongo tu ina maana watu wangekuwa wanapata taarifa tu na kubainisha kuwa kunahitajika watu kama kina Ruge kina Mengi, Diamond, Chid Benzi na wengine.

Soma zaidi: VIDEO: Mwili wa Ruge kuwasili Ijumaa, kuzikwa Bukoba Jumatatu

 



Chanzo: mwananchi.co.tz