Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chid Benz, Juma Nature wageuka kivutio Tigo Fiesta

33078 CHID+PIC Chid Benz

Sun, 23 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Licha ya kutotoa ngoma kwa muda mrefu, wasanii Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ na Juma Kassim ‘Juma Nature’ wameonekana kivutio katika tamasha la Tigo-Fiesta.

Tamasha hilo ambalo lilifanyika jana Jumamosi na kumalizika leo saa 12 asubuhi Jumapili ya Desemba 23, 2018 katika viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam lilishirikisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya na bendi.

Pamoja na uwepo wa wasanii wengi wanaokadiriwa kufika 30, wasanii Juma Nature na Chid Benzi waliopanda saa 6:00 hadi 7:45 jukwaani walionekana kivutio ukilinganisha na wasanii wengine.

Kwa upande wa Chid Benzi watu walionekana kumshangilia ukizingatia ni hivi karibuni alionekana katika mitandao ya kijamii akiponda kitendo cha yeye kuachwa kwenye tamasha la Wasafi pamoja na kuwa msanii mzuri.

Kama vile haitoshi msanii huyo aliweza kuonyesha kuwa uwezo wake wa kuchana mistari uko palepale na pumzi ya kutosha kuhimili jukwaa kwa muda mrefu.

Kila kibao alichokuwa akiimba Chid Benz alikuwa akishangiliwa mwanzo mwisho, huku akiwakumbushia nyimbo alizowahi kutamba nazo katika muziki wa bongo fleva ikiwemo Dar es Salam Stand Up, Raha za Dunia, Niite Chid na nyinginezo.

Naye Juma Nature aliweza kuwakumbusha vibao mbalimbali watu waliohudhuria tamasha hilo, ikiwemo sitaki demu, kamua,  everybody stand up, ugali, Asia na vinginevyo ambapo kila alipotaka kushuka jukwaani watu walitaka aendelee.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz