Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Charlemagne Tha God aiponda ngoma ya Drake

Wed, 22 Apr 2020 Chanzo: --

MTANGAZAJI nyota nchini Marekani, Charlemagne Tha God, ameuponda wimbo mpya wa Drake, Toosie Slide akidai upo chini ya kiwango.

Tha God, amekiambia kipindi cha The Brilliant kuwa licha ya mafanikio ya wimbo huo kwenye mitandao mbalimbali anaona haujafika kiwango cha Drake.

“Ukiwa rapa mkubwa duniani hautakiwi kufuata kiki, sijauheshimu wimbo wake sio mzuri, naona wanaucheza, hizi ni nyimbo zile ambazo zinapendwa kwasababu ya kitu fulani, Drake amejitengeza kama mtu ambaye hatakiwi kufanya hiyo,” alisema Tha God.

Drake aliachia wimbo Toosie Slide wiki mbili zilizopita na ukafanikiwa kutikisa chati mbalimbali huku kwenye mtandao wa TikTok ukitazamwa na watu bilioni 3 kutokana na mtindo wake wa kucheza.

Chanzo: --