Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chanzo wimbo wa Dayoo kuwekwa kwenye YouTube ya Rayvanny

Chanzo Wimbo Wa Dayoo Kuwekwa Kwenye YouTube Ya Rayvanny Chanzo wimbo wa Dayoo kuwekwa kwenye YouTube ya Rayvanny

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kuwa Dayoo amemshirikisha Vanny Boy kwenye wimbo wake 'Huu Mwaka Remix'lakini video ya wimbo huo upo kwenye YouTube chaneli ya Rayvanny ambaye kashirikishwa tu, Dayoo anasema hilo limetokea na makubaliano yao ya kibiashara.

"Makubaliano yote kati yetu yapo kwenye mikataba, hivyo sitapenda kuliongelea sana maana vitu vipo kwenye mikataba tayari kwa maslahi ya pande zote mbili." Anasema

Aidha Dayoo ameeleza awali alimtumia Rayvanny wimbo wa 'Huu mwaka' ili washirikiane, lakini ulipotoka na kupata mapokezi mazuri ndani ya muda fupi ndipo uliongeza ushawishi kwa Rayvanny akakubali kushiriki kwenye remix.

"Rayvanny ndiye msanii wa kwanza ambaye nilimtumia kabla hata wimbo wenyewe haujatoka, baadaye ulipotoka na kuanza kufanya vizuri katika mitandao ya kijamii akaupenda, hivyo ikawa rahisi kufanya naye kazi," anasema Dayoo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live