Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chanzo chatajwa Vifo 11 kwenye tamasha la Travis Scott

Travis Baadhi ya Mashabiki waliohudhuria tamasha

Sat, 6 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa mpya iliyotolewa baada ya uchunguzi wa awali juu ya chanzo cha vifo katika tamasha la Muziki la Travis Scott zinasema kuna mtu mmoja miongoni mwa waliohudhuria alirukwa na akili na kuanza kuwachoma watu Sindano yenye kuaminika kwamba ilikuwa na chembe za madawa ya kulevya.

Jambo hilo ndilo lililokuwa chanzo cha kuibua zogo kiasi cha watu wengi kuanza kusukumana, kitendo kilichopelekea watu kuanza kukanyagana, kubanana kiasi cha wengine kukosa pumzi na kufariki huku wengime kadhaa kukimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi.

Kwa mujibu wa TMZ inasemekana baadhi ya watu walipatikana wakiwa wamefariki kwa kile kinachodaiwa kuwa walipatwa na shambulio la moyo kitu kinachopelea kuhisiwa kwamba pengine walichomwa sindano na mtu huyo.

Aidha Travis Scott ametoa kauli rasmi kufuatia tukio hilo kwa kuweka bayana kuwa ameshtushwa sana na tukio hilo na anatoa pole kwa familia za wahanga wa tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live