Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chanzo cha kifo cha Mzee wa Mjegeje chatajwa

Kata Simu 2 Mjegeje Chanzo cha kifo cha Mzee wa Mjegeje chatajwa

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Thabiti Ally Kipwasa ‘Real Jimmy’ ambaye ni Meneja wa aliyekuwa msanii wa Bongo, Mzee Omar maarufu kama Mzee wa Mjegeje amefunguka kwamba chanzo cha kifo cha msanii huyo ni maradhi ya bandama na figo yaliyokuwa yakimsumbua.

Thabiti ameongeza kuwa, Mzee wa Mjegeje alitoa kauli kuwa akifa asizikwe nyumbani kwao Bagamoyo, badala yake azikwe Dar es Salaam kwa sababu ndugu zake wote walimkataa wakati akiugua.

“Mzee alikuwa anaumwa serious sana tukampeleka Hospitali ya Palestina (Sinza). Ameanza kuugua kama mwezi mmoja hivi uliopita akisumbuliwa na bandama na figo, mi miguu ilianza kuvimba.

“Nilipambana kwa kadri navyoweza lakini kwa sababu sina kipato cha kutosha, tukawacheki ndugu zake, wakamkataa kipindi anaumwa. Mwanaye Shufaa anajua kila kitu kinachoendelea na nilikuwa nampa taarifa kila kitu kuhusu hali ya mzee.

“Lakini leo kafa, ndugu zake wanajitokeza wanataka mwili. Mimi niliweka rahani mpaka vitu vyangu ili mzee apate matibabu," amesema Thabiti.

Mzee wa Mjegeje aliyetamba kwenye mitandao ya kijamii kwa video yake ya 'Kata simu tupo site' amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Machi 20, 2024 katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matoiabu.

Mzee wa Mjegeje alikuwa msanii kutoka Bagamoyo, Tanzania ambaye alikuwa akijihusisha na shughuli zote za sanaa hasa za maigizo ya vichekesho na uimbaji wa muziki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live