Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Channel za Bure Kurudishwa DStv

Dstv12 Channel za Bure Kurudishwa DStv

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Habari Nape Nnauye leo ametangaza rasmi kurudishwa kwa TV channels za bure kwenye king’amuzi cha DSTV mfano CloudsTV, ITV n.k baada ya kutembelea ofisi za Multichoice Tanzania (DStv) jijini Dar es salaam.

“Moja ya maagizo ya Mh. Rais Samia ni kuboresha mawasiliano, sasa katika maboresho tunazo baadhi ya kanuni, sera na sheria ambazo inabidi tuwe tunazibadili mara kwa mara ziendane na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia duniani” amesema Nape.

“Leo pamoja na kuwashukuru DSTV Tanzania kwa kazi nzuri mliyofanya na kutambua mchango wenu kwenye sekta yetu nikasema leo nitangaze moja ya mabadiliko tuliyoyafanya kwenye kanuni zetu, kuna kanuni namba 18 ya mwaka 2018 inayohusiana na miundombinu ya utangazaji wa kidigitali, tumeifanyia marekebisho ili kuruhusu Channel za TV ambazo hazilipiwi (mfano CloudsTV, ITV n.k) ziweze kuonekana kwenye king’amuzi cha DSTV”amesema Nape.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live