Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Chai tamu ni ile ilioongezwa chumvi - Mwanasayansi

Chai Tamu Ni Ile Ilioongezwa Chumvi   Mwanasayansi Chai tamu ni ile ilioongezwa chumvi - Mwanasayansi

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: bbc

Waingereza wanadai kujua jambo moja au mawili linapokuja suala la kutengeneza kikombe kizuri cha chai.

Kinywaji hicho ni taasisi ya kitamaduni nchini Uingereza, ambapo wastani wa vikombe milioni 100 hunywewa kila siku.

Lakini sasa mwanasayansi aliyeko zaidi ya maili 3,000 nchini Marekani anadai kuwa amepata siri ya kikombe kizuri cha chai ambacho Waingereza wengi hapo awali wangeona upuuzi kabisa - kuongeza chumvi.

Utafiti wa Prof Michelle Francl umezua taharuki kubwa nchini Uingereza, na hata umevutia uingiliaji kati wa kidiplomasia kutoka kwa Ubalozi wa Marekani.

"Tunataka kuwaelezea watu wa Uingereza kwamba wazo hili lisilofikirika la kuongeza chumvi kwenye kinywaji cha kitaifa cha Uingereza sio sera rasmi ya Marekani.

Na haitakuwa hivyo," ubalozi ulisema kwenye X, ambayo zamani ilijulikana kama Twitter.Sio mara ya kwanza kwa kinywaji hicho kusababisha mabishano pande zote mbili za Atlantiki.

Hapo awali 1773, waandamanaji huko Boston, Massachusetts ya kikoloni, walitupa kreti 300 zilizojaa chai kwenye bandari kupinga ushuru wa Waingereza - wakati muhimu ambao ulichochea Mapinduzi ya Amerika.

"Hakika sikukusudia kusababisha mvutano wa kidiplomasia," Prof Francl, profesa wa kemia katika Chuo cha Bryn Mawr huko Pennsylvania, aliambia BBC.

"Barua pepe zangu zimekuwa zikisababisha wazimu leo. Sikutarajia kuamka asubuhi hii kuona watu wengi wakizungumza kuhusu chumvi kwenye chai yao."lakini kwa nini kuongeza chumvikatika chai?

Ilibainika kuwa si wazo geni - kiungo hicho kimetajwa hata katika hati za Kichina za karne ya nane, ambazo Prof Francl alizichanganua ili kukamilisha mapishi yake."Kilicho kipya ni kuelewa kwetu kama wanakemia," Prof Francl alisema.

Anaeleza kuwa chumvi hufanya kazi ya kuzuia kipokezi jambo ambalo huifanya chai kuwa chungu hasa inapopikwa.Kwa kuongeza chumvi ya mezani - kiasi kisichoweza kutambulika - utakabiliana na uchungu wa kinywaji."Siyo kama kuongeza sukari.

Nadhani watu wanaogopa chai yenye chumvi."Anawahimiza Waingereza wanaopenda chai kuwa na mawazo wazi kabla ya kuhukumu mapema utafiti wake, ambao ameuandika katika kitabu chake kipya cha Steeped: The Chemistry of Tea, kilichochapishwa na Jumuiya ya Kifalme ya Kemia.

Chanzo: bbc