Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Celine Dion aahirisha maonesho yote kwa sababu ya afya mbaya

Celine Dion Aahirisha Maonesho Yote Kwa Sababu Ya Afya Mbaya Celine Dion aahirisha maonesho yote kwa sababu ya afya mbaya

Sun, 28 May 2023 Chanzo: Bbc

Celine Dion ameahirisha maonesho yake yote ya moja kwa moja yaliyosalia, akiwaambia mashabiki hana nguvu za kutosha za kutembelea baada ya kugunduliwa na ugonjwa wa neva.

Mwimbaji huyo alifichua mwaka jana kwamba alikuwa akiugua ugonjwa wa Stiff-Person Syndrome (SPS), ambao ulikuwa ukiathiri uimbaji wake.

Dion sasa ameghairi maonesho yote ambayo alikuwa amepanga kwa 2023 na 2024. Katika taarifa iliyotumwa kwenye Twitter, mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 55 aliwaambia mashabiki: "Samahani sana kuwakatisha tamaa nyote kwa mara nyingine tena.

"Ingawa inaniumiza moyo, ni bora tughairi kila kitu hadi nitakapokuwa tayari kurejea jukwaani." Aliongeza: "Sikati tamaa... na siwezi kusubiri kukuona tena!"

Mnamo Desemba 2022, mwimbaji huyo wa Ufaransa na Canada alichapisha video ya hisia kwenye Instagram kusema kuwa amegunduliwa na SPS na hangekuwa tayari kuanza ziara ya Ulaya mnamo Februari kama ilivyopangwa.

Alisema ugonjwa huo ulikuwa ukisababisha kukakamaa kwa misuli na "hakuniruhusu kutumia sauti kuimba jinsi nilivyozoea". Ziara ya Ulimwengu ya Ujasiri ilianza mnamo 2019, na Dion alikamilisha maonyesho 52 kabla ya janga la Covid-19 kusimamisha iliyobaki.

Taarifa iliyotolewa na ziara yake ilisema maonesho hayo yalikuwa yameahirishwa kwa "hisia ya kukatishwa tamaa sana". "Ninajitahidi sana kurejesha nguvu zangu, lakini utalii unaweza kuwa mgumu sana hata ukiwa na asilimia 100," taarifa hiyo ilimnukuu Dion akisema.

Ziara hiyo ingekuwa ziara ya kwanza ya Dion ya kimataifa katika muongo mmoja na ya kwanza bila mume wake meneja Rene Angelil, ambaye alikufa kutokana na saratani mnamo 2016. Dion anafahamika zaidi kwa vibao vikiwemo My Heart Will Go On, Because You Loved Me, All By Myself na It's All Coming Back To Me Now

Chanzo: Bbc