Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cassper Nyovest: Nilikuwa mzinzi lakini nimemrudia Mungu

Cassper Nyovest South Cassper Nyovest

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapper wa Afrika Kusini, Cassper Nyovest amefichua kuwa upendaji wake wa ngono uliopita kiasi ndio chanzo cha yeye kuachana na mama watoto wake, Thobeka Majozi.

Ikumbukwe kuwa wawili hao wana mtoto wa kiume waliyempata Septemba 2020.

Akiongea kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni kwenye Podcast ya Mpoomy Ledwaba, Cassper alikiri kuumiza hisia za mama watoto wake walipokuwa kwenye mahusiano.

Hata hivyo, alifichua ya kwamba kwasasa ameokoka na ameamua kumrudia mungu wake.

"Nilimuumiza sana mama mtoto wangu. Tuliachana na nimekuwa single kwa miaka miwili, Nilikuwa muasherati na mbinafsi mkubwa na nilijiona kuwa bora kuliko wengine" rapper huyo alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live