Licha ya kuwa kwenye bifu kwa miaka 9, Cassper Nyovest amemsindikiza marehemu AKA kwa maneno ya upendo. Baada ya wasanii na mashabiki wa Muziki barani Afrika kuandika maneo yao ya faraja, alibaki Cassper ambaye naye amefunguka haya;
“Kwa mashabiki zangu wote, tafadhali tumeni salamu zenu za upendo kwa Megacy (AKA) na familia yake. Taifa linaomboleza na tunaweza kutumia upendo zaidi kuliko chuki.” ilisomeka Tweet ya kwanza ya Cassper.
Tweet yake ya pili ilifuata saa 9 mchana ikisema “Salamu zangu pole ziende kwa familia ya Kiernan na Tebello, watu wa karibu na mashabiki.
Roho zao zimpumzike kwa amani na urithi wao uzidi kusheherekewa. Mungu wetu mwema awe na nanyi katika nyakati hizi za majonzi.”