Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Caren Simba adaiwa kunasa penzi na Fred Vunjabei

Vunjabei Caren Simba Caren Simba na Fred Vunjabei

Wed, 28 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii maarufu wa Bongo Movie, Caren Simba amejikuta katika wakati mgumu huku akiogelea matusi ya mashabiki zake baada ya kuhusishwa kuzama penzini na mfanyabiashara maarufu nchini, Fred Vunjabei.

Hii inakuja baada ya Caren Simba mwenyewe kumpost Fred Vunjabei na kusindikiza na maneno machache yaliyowapa watu nafasi ya kudhani kuwa wawili kwa sasa wapo kwenye huba zito.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram (Insta Stori), Caren ameandika; "Forever Partner in Crimes @fred_vunjabei," yanasomeka maneno hayo.

Ikumbukwe hivi karibuni, Fred Vunjabei alitangaza kuwa mwezi huuu ataingia tena kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live