Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Caren Simba: Harmonize alitongoza lakini...

Careen Simba Harmo Caren Simba na Harmonize.

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji wa Kibongo Caren Simba amesema hajawahi kuwa kwenye mahusiano na Staa wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Harmonize kama watu wanavyomdhania, huku akifafanua kuwa kilichoonekana ilikuwa ni kazi na baada ya kazi kuishi walibaki kuwa washkati wakushibana.

Caren amesema yupo kwenye mahusiano na mpenzi wake japokuwa ni kweli Harmonize aliwahi kumtongoza lakini ilimuwia vigumu kwa sababu tayari alikuwa kwenye mahusiano na mwanaume mwingine ambaye yupo naye mpaka sasa.

Aidha, Caren ambaye ni video vixen wa ngoma ya 'Single Again' amesema Harmonize siyo mtu mbaya na hata kipindi anatongozwa kama asingekuwa na mwanaume mwingine angekubali kuwa na Harmonize.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live