Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cardi B agoma kupiga kura kisa Trump na Biden

Cardi B Come Again Cardi B agoma kupiga kura kisa Trump na Biden

Fri, 17 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

‘Rapa’ kutoka Marekani Cardi B amedai kuwa hatapiga kura katika uchaguzi ujao nchini humo huku akimkataa Rais Joe Biden na mpinzani wake Donald Trump.

Cardi akiwa kwenye mahojiano na ‘Rolling Stone out’ siku ya jana Alhamis, Mei 17, 2024 ameweka wazi sababu ya kutokupiga kura kwa kudai kuwa anaona watu wa Marekani wamesalitiwa kutokana na gharama kubwa za maisha na mishahara midogo.

Hata hivyo mwanadada huyo aliongea machache kuhusu aliyekuwa Rais wa nchi hiyo #DonaldTrump kuwa asingependa aingea madarakani kutokana na kuiingiza Marekani kwenye shida.

Ikumbukwe kuwa jCardiB katika uchaguzi uliyopita mwaka 2020 akwenda kumpigia kura Rais aliyekuwa madarakani Joe Biden kutokana na sera zake za kurahisisha maisha kwa Wamarekani. Uchaguzi mkuu #Marekani wa 2024 unatarajiwa kufanyika Jumanne Novemba 5, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live