Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Calisah afunguka sakata la kupigwa na Nay wa Mitego

Calisah Na Nay Calisah afunguka sakata la kupigwa na Nay wa Mitego

Wed, 20 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamitindo Calisah amefungukia sakata la kupigwa na msanii wa Bongo Fleva Nay wa Mitego lililotokea kwenye viwanja vya Mlimani City jijini Dar.

Akizungumza na Wasafi FM, Calisah amesema, siku ya tukio, Nay alikuwa na washkaji zake na kumfanyia fujo lakini bahati ilikuwa kwake kwani alikuwa na washkaji zake wakamkingia kifua kisha yeye akasepa.

“Aliponianza mimi nilizunguka kwa mbele watu wakajua nimemuogopa kumbe mimi nilikwenda ili tukakutane naye uso kwa uso sasa wakati namkaribia, washkaji zake wakanizonga nikaanguka chini, nilipoanguka akaja Nay kunikanyaga mateke mawili usoni,” alisema Calisah na kuongeza:

“Kinachoniuma mimi bora hata angenipiga tukiwa wawili ningesema poa ameshinda lakini pale ni kama alitaka tu kujichukulia pointi tatu halafu akakimbia, kwangu mimi naona ananiogopa.”

Calisah anasema hata hivyo alimfuata Nay studio kwake kisha akaenda kulifikisha suala hilo polisi kwa ajili ya hatua zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live