Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yafafanua matibabu wasanii Belle 9, Lulu Diva kupata ajali

1070ecc84479365e1a717f2e4d2765f4 CCM yafafanua matibabu wasanii Belle 9, Lulu Diva kupata ajali

Mon, 7 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa kinafuatilia kwa ukaribu na kuhakikisha wasanii watatu ambao ni Luludiva, Belle9 na Bonge la Nyau ambao wamepata ajali hii leo wakati wakitokea mkoani Iringa wanapata matibabu haraka.

Taarifa ya CCM iliyotolewa leo Septemba 7, 2020, kupitia ukurasa wake wa Twitter ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Hamphrey Polepole imeeleza, "Chama Cha Mapinduzi tumepokea kwa mshtuko taarifa za ajali mbaya ya gari iliyowahusisha wasanii Belle9, Lulu Diva na Bonge la Nyau, tunafuatilia kwa ukaribu kuhakikisha wanapata huduma ya matibabu haraka na tunamwomba Mungu awape wepesi na kupona haraka.”

Wasanii hao wamepata ajali majira ya alfajiri hii leo, katika eneo la Chalinze wakati wakitokea Iringa, huku chanzo wakieleza kuwa ni Lori kuwachomekea kwa mbele, ndipo dereva wao akalitumbukiza gari kwenye korongo ili wasigongane uso kwa uso.

Kuhusu taarifa za ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jonathan Shana alilieleza kuwa wanafuatilia tukio hilo na watatoa taarifa hapo baadae.

Kwa upande wake, akizungumza Lulu Diva amesema amepata majeraha upande wa kichwa, ambapo ameeleza kuwa msanii mwenzie Belle 9 ndiye ambaye anaonekana kuumia zaidi

“Ni kweli tumepata ajali mimi nimeumia kichwani ila aliyeumia zaidi ni Belle 9 na amekimbizwa hospital kwa matibabu zaidi mimi nimevimba kichwani Bonge la nyau ameumia kiasi…

“Mpaka sasa bado sijajua chanzo cha ajali kwa sababu nilikuwa nimelala wakati ajali inatokea nikaja kushtuka gari imeacha barabara na kupinduka ila Bell 9 anaonekana kuumia Mgongo na maeneo ya Kichwani,” amesema Diva mapema leo hii

***Bado tunaendelea kufatilia zaidi habari hii kwa undani, tutawajuza.

Chanzo: habarileo.co.tz