Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Bwana harusi aua wanne akiwemo bibi harusi

Bwana Harusiii Bwana harusi aua wanne akiwemo bibi harusi

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watano wamefariki dunia nchini Thailand baada ya bwana harusi kuwashambulia watu wanne kwa risasi akiwemo bibi harusi na baadaye kujifyatua mwenyewe.

Askari wa zamani na mwanariadha Chaturong Suksuk (29) alimuua mke wake Kanchana Pachunthuek (44) masaa machache baada ya wawili hao kufunga ndoa.

Tukio hilo lilitokea, baada ya bwana harusi kuondoka ghafla kwenye sherehe ya harusi Jumamosi usiku na baadaye kurudi na bunduki.

Wengine aliowapiga risasi na kuwaua ni pamoja na mama mkwe wake, shemeji yake ambaye ni dada wa bibi harusi, na mgeni mualikwa mmoja.

Wageni wa harusi hiyo wameeleza kuwa walimuona bwana harusi akiwa hana furaha wakati wa sherehe.

Kwa mujibu wa Polisi, Chaturong alikuwa amelewa sana, hata hivyo sababu ya kile alichokifanya haieleweki.

Mapema mwaka jana, aliinunua bunduki hiyo pamoja na risasi kwa kufuata sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live