Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Busta: Burna Boy anajua anachokifanya kwenye muziki

Busta: Burna Boy Anajua Anachokifanya Kwenye Muziki Busta: Burna Boy anajua anachokifanya kwenye muziki

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani, Busta Rhymes amesema kufanya kazi na msanii kutoka Nigeria, Burna Boy umekuwa ni wakati bora katika maisha yake ya muziki.

Aidha, mkongwe huyo wa muziki wa Hip-hop amesema anapenda vitu vingi kutoka kwa msanii huyo wa Afrobeat ikiwemo uharaka na ufanisi wake kwenye kazi.

Hata hivyo, Busta akiwa katika mahojiano nchini Marekani amethibitisha kufanya 'kolabo' na Burna huku sababu kubwa ya kufanya naye kazi ameeleza ni kwa sababu Burna anajua anachofanya katika muziki.

Busta ameachia kibao chake kipya kiitwacho ‘BIG EVERYTHING’ ambacho hadi leo ni siku ya tatu tangu akiachie huku kwenye mtandao wa YouTube tayari kimetembelewa na watazamaji milioni moja, katika 'Big Everything' amewashirikisha wasanii DaBaby na T-Pain.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live