Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burna Boy kashindikana! Sasa kushusha kitu kizito na Dj Khaled

Burna Boy Na Dj Khaled.png Burna Boy na Dj Khaled

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshindi wa Tuzo ya Grammy kutoka pande za Nigeria, Damini Ebunoluwa Ogulu maarufu kama Burna Boy tayari amezama Studio na Producer maarufu ulimwenguni na mwanamuziki kutoka nchini Marekani, Khaled Mohamed Khaled ‘DJ Khaled’.

The African Giant anatengeneza ngoma hiyo na Khaled katika moja ya studio kubwa nchini Marekani lakini bado jina la ngoma hiyo halijaanikwa.

Katika video mbalimbali ambazo Burna Boya na Khal;ed wameposti kila mmoja kwenye mitandao yake ya kijamii, zinamwonyesha Burna Boy akirekodi wimbo huku Dj Khaled akicheza wimbo huo.

Mashabiki wa mastaa hao sasa wategemee bonge moja la project kutoka kwa producer huyo mkubwa duniani sambamba na mfalme wa Afrobeats kutoka nchini Nigeria.



Ikumbukwe pia kuwa, hivi karibuni mtandao mmoja mkubwa nchini Nigeria uliripoti kuwa muda wowote mashabiki wategemee kolabo kati ya Burna Boy na Dj Khaled.

Kupitia ukiurasa wake wa Instagram, DJ Khaled jana Jumanne, Oktoba 11, 2022 aliposti kipande cha video akiwa studio huku sauti yake ikisikika akiimba na kucheza wakati huo akiweka caption akionyesha kujifananisha na Burna Boy; “Moto mkali unazidi kuunguza, unaweza kudhani mimi ni @burnaboygram ???????????????????????? ????” aliandika Khaled.

View this post on Instagram

A post shared by DJ KHALED (@djkhaled)



View this post on Instagram

A post shared by DJ KHALED (@djkhaled)



View this post on Instagram

A post shared by DJ KHALED (@djkhaled)



View this post on Instagram

A post shared by DJ KHALED (@djkhaled)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live