Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burna Boy kama Harmonize tu

Harmonize Na Burna Boy Burna Boy kama Harmonize tu

Wed, 20 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa wale tuliosoma Cuba nahisi tumeelewa haya matukio mawili ya Burna Boy na Harmonize ya kuhonga mandinga kwa wanawake zao baada ya kutengeneza ngoma kubwa (Hit Songs) kupitia maudhui (content) ya wanawake zao wa zamani.

Ukija kwa upande wa Harmonize utagundua kuwa Kajala (Ex) wake ndio sababu ya kuandika wimbo wa Single Again ambao umekuwa na matokeo makubwa sana na faida kwa Harmonize kiasi kwamba sio swala kabisa hata ile Range aliyomuachia mtoto kwasababu ameingiza mitonyo kupitia ngoma aliyoandika kumuhusu.

Ukirudi kwa Burna Boy pia juzi hapa amempa Ex wake ,Stefflon Don, zawadi ya ndinga aina ya Rolls-Royce Cullinan ambayo kimsingi na yeye Burna Boy ni kama amerudisha tu kwa jamii maana amepiga mitonyo mingi sana kupitia ngoma ya "Last Last" ambayo aliandika kwa lengo la kumchana Ex wake huyo, na ni wimbo ambao Burna anasema ulimuingizia pesa mingi sana ndani ya muda mfupi.

Hivi jamani ni Burna Boy ndio yupo kama Harmonize au ni Harmonize ndio yupo kama Burna Boy maana ukiachana na unyama wao wa kufanya mziki mzuri ila ni wana ambao wana matukio flani flani hivi yanayofanana kwenye maisha yao ya ndani na nje ya mziki.

Dondosha Comment yako.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live