Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burna Boy ana jambo lake hivi karibuni

Burna Boy Has Postponed His Concert At FNB .jpeg Burna Boy

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkali wa Afrobeat kutoka #Nigeria, Burna Boy amedai kuwa ngoma yake ijayo ndio itakuwa ngoma bora kushinda ngoma zote zilizotoka mwaka huu.

Mwanamuziki huyo ameyasema hayo kwenye mahojiano yake wakati alipokuwa kwenye onesho la mitindo la ‘Paris Fashion Week’ ambapo aliweka wazi kuwa kuna nyimbo ameirekodi siku mbili zilizopita huku akiamini kuwa ndio itakuwa bora kushinda zote.

Kwa sasa #BurnaBoy anatamba na ngoma ya ‘#TshwalaBamRemix’ aliyoshirikishwa na #TitoM, #Yuppe ambapo mpaka kufikia sasa ina zaidi ya watazamaji milioni 7.9 kupitia mtandao wa YouTube.

Katika onesho hilo la mitindo lililofanyika Jana jijini Paris nchini Ufarasa mwanamuziki huyo alifanikiwa kutumbuiza ngoma zake mbalimbali ikiwemo ‘Tshwala Bam Remix’ kwenye Party iliyoandaliwa na ‘Paris Fashion Week’.

Mastaa wengine ambao walifanikiwa kuhudhuria katika maonesho hayo ni #Rema, #Wizkid, #Maluma, #SwaeLee na wengineo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live